Jumapili, 29 Januari 2017

BOND ALAZIMIKA KUACHANA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI ILI ASIMKOSE MREMBO WASTARA

Msanii wa filamu Wastara Juma amefunguka zaidi  kwa kudai kuwa moja kati ya sababu  ambayo ilichangia akaachana na mpenzi wake wa sasa Bond Bin Sinan na  kuolewa na mwanaume miwngine, ni matumizi ya mirungi pamoja na pombe


.Hatua hiyo ilimfanya Bond kujiuliza mara mbili mbili na ndipo alipoamua kwenda rehab kuachana na ulevi huo ili apate nafasi ya kurudi kwa malkia huyo wa filamu.
Wastara alidai ulevi huo wa Bond ulimsababisha yeye asiwe na furaha na kuamua kumuacha ili aendelee na maisha yake.
“Ukweli ni kwamba kuna issue nzito ilitokea kati ya mimi na Bond mpaka Bond mwenyewe aliamua kutoa ushuhuda na kutubu juu ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi,” Wastara alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.
“Mpaka aliamua kuondoka mwenyewe kwenda mbali na mazigira ambayo mimi nilikuwa naishi, alikuwa anatafuta njia ya kujisaidia ili aache vile vitu ambavyo binafsi nilikuwa sivipendi,” aliongeza Wastara.

Muigizaji huyo amedai baada ya tukio hilo alishauriwa na ndugu zake kuolewa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma lakini ndoa hiyo haikudumu wakaachana.
Kwa sasa Bond na Wastara wamerudiana na wanaendelea na mahusino yao baada ya Bond kufanikiwa kuachana matumizi hayo ya Madawa ya kulevya aina ya mirungi.

ALIKIBA

Ali Saleh Kiba maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania,wanazidi kufanya vizuri na kupeleka muziki wa hapa bongo Afrika Mashariki na pengine Dunia nzima kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.


Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo  mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda tuzo mbalimbali  ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda na inazidi kupanda maradufu barani Afrika na pengine, kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, pamoja  kazi zake, ni wapi ametoka, alipo sasa, na wapi anakwenda.
Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention zaidi kwenye soko la muziki barani Afrika.
Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.

Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa, wasanii wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki kabla ya kuachia kazi zao mpya ili kupata attention. Nafahamu kuwa msanii Alikiba amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi ambazo zinajitengeneza zenyewe ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia kibiashara sababu kuna wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini hawazipati.
Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour yake itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour yake inaanza February mwaka huu. Hivyo mpaka ninaandika makala hii zimebaki siku tatu kufikia mwezi February.
Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki barani basi ni Afrika Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea Diamond Platnumz kwenye kiwanda cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya collaboration na AKA ili kupenyeza muziki wake África Kusini.
Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi na namna ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la mUziki linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram msanii wa maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost kipande cha screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine wa Alikiba DM kua Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha wanayoitaka, siku zote amekuwa mtu wa kujiamini na kuwasibirisha mashabiki wake ambao ukweli bila wao asingekua hapo halipo leo.
Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti kwa kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya iwe ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi husika? Aliahidi atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii kutoka Nigeria MI Abaga lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna dalili ya hiyo nyimbo?

Binafsi nilidhani ingekuWa sahihi sana kama angeachia nyimbo ambayo amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la kuiteka zaidi South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata wakati wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya media tour kuitambulisha zaidi hiyo ngoma.

Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu yuko kasi lakini naona Alikiba bado yule yule.

GENEVIVE MISS TANZANIA 2010 AMEACHIA NGOMA YAKE YA NANA


 Genevieve Emmanuel amabe alikuwa miss Tanzania 2010 nae ameingia katika orodha ya wasani kwa kutoa ngoma yake mpya ya nana ambayo inatrend sanagoma hiyo imetayarisha na Luffa.


Dondoka youtube uwe wa kwanza kuisikila  nyimbo ya Genevive Emmanuel Miss Tanzania 2010

Ijumaa, 13 Januari 2017

AKOTHEE AMEFUNGUKA JUU YA TETESI YA KUMLIPA DIAMOND MIL 36

Muimbaji wa Kenya, Akothee amefunguka tetesi zilizosambaa sana kuwa alimlipa Diamond Platnumz kiasi cha shilingi milioni mbili za Kenya ili ashiriki katika wimbo wake wa ‘Sweet Love’. Kiasi hicho ni takriban shilingi milioni 36 za Tanzania.



Akiongea katika kipindi cha runinga cha Talk Central cha K24, Akothee amekataa kuweka wazi lakini amedai kuwa fedha hiyo ni kitu kidogo kwa kuwa na kama wimbo huo usingekuwa mzuri wangeomba warudishiwe fedha yao.
“What is two million shillings? No! am not saying no but am not saying yes, am saying why 2 million. Is the song good, we don’t have to talk about price if the song is not good then if we have paid we will ask our money back,” amesema Akothee.
“And now the song is doing well let’s just talk about the song,’ ameongeza.

Mpaka sasa wimbo huo umefanikiwa kutazamwa mara 3,383,577 kwenye mtandao wa YouTube na umekuwa wimbo wa kwanza wa muimbaji huyo kutazamwa zaidi katika mtandao huo.

MAJANGA YAMKUTA SOULJA BOY AKIJIANDA NA PAMBANO NA CHRIS BROWN

Wakati wa maandalizi ya pambano lake la ngumi kati ya Chris Brown, majanga yameanza kumkuta rapper Soulja Boy.


Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Jumanne hii nyumba ya rapper huyo iliyopo Hollywood Hills ilivamiwa na mwizi aliyefanikiwa kuondoka na fedha kiasi cha $10,000, pamoja na vitu vyenye thamani ya $12,000.

Hata hivyo imedaiwa kuwa kamera zilizofungwa katika eneo hilo zimefanikiwa kupata picha ya mwizi huyo ambapo polisi wanaendelea na umfuatiliaji. 
Japo kumekuwa na mvutano juu ya pambano lake na Chris Brown lakini hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuwa wizi huo umefanywa na watu wa upande wa Chris kama kumchanganya Soulja 


JOH MAKINI KUBEBWA KISANAA SIJASEMA KWA UBAYA- YOUNG KILLER


Msanii wa muziki wa hip hop Young Killer anadaiwa kumdiss Joh Makini  msanii wa Hip Hop kwenye wimbo yake mpya ‘Sina Swaga’ akidai kwamba anabebwa sana kisanaa


“Mimi sijaiongea kwa ubaya, nimeielezea kwa sababu hata Chidi Benz alishawahi kuizungumzia, lakini Joh kwangu ni msanii ambaye namkubali na kama nikisema nimweke kwenye list, tatu bora yupo,” Young Killer alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV

Pia rapper huyo alidai kuwa kuna ushaidi mwingi wa picha kwenye blog tofauti zinazoonesha jinsi Joh anavyotuhumiwa kubebwa kisanaa na kusema hana tatizo na Joh Makini na hata akikutana naye atamsalimia.

ALPHA KUTAJA NYIMBO KADHAA AMBAZO HUSIKILIZA ZAIDI

Mshindi wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa 3, Alpha Rwirangira alifanikiwa moja ya ndoto kwa kuhitimu shahada yake ya kwanza katika fani  yake ya Masoko na Muziki December 2015


.Ameendelea kukaa nchini humo huku akiendelea kufanya shughuli zake na pia muziki hajauweka kando. Muimbaji huyo amezitaja nyimbo kadhaa ambazo anazisikiliza zaidi kwa sasa kuwa ni:

5. Dume Suruali – Mwana FA f/ Vanessa Mdee
4. Aje – Alikiba
3.Salome – Diamond Platnumz f/ Ray Vanny
2.Muziki – Darassa
1.Ya Mungu – yake mwenyewe