FAHAMU MATUNDA MATANO YANAYOWEZA KUFANYA NGOZI YAKO IWE KATIKA MUONEKANO MZURI.
Katika maisha watu wamechukulia mazoea sana katika ulaji wa matunda na kutotilia maanani bila kujua kuwa matunda ni muhimu sana katika miili yetu, na yanatukinga na magonjwa pia kuipa ngozi yetu muonekano mzuri kila siku.
Kwahiyo kuna kila sababu ya kukubali kuwa matunda yana umuhimu katika miili yetu kwasababu yanaongeza vitamini zifuatazo;
PARACHICHI; Ni tunda ambalo ni maarufu sana na linatumika katika kutengeneza juisi, tunda hili lina vitamini za kutosha ambapo huongeza mafuta mwilini, kwa wanaopenda kulitumia inashauriwa kula au kunywa juisi ya parachichi hususani kama huna tatizo la kuzidi kwa mafuta mwilini. Pia Parachichi huongeza uzito endapo utalitumia mara kwa mara
PAPAI; Hili ni tunda moja wapo ambalo linaweza kung'arisha ngozi yako na kuifanya iwe na muonekano mzuri, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana na papai itwayo 'papain,' endapo kama utahitaji kusafisha uso wako ni vizuri kutumia papai lililo iva changanya na asali itasaidia uso wako kuwa katika muonekano mzuri.
CHUNGWA; Tunda hili linasaidia kurejesha ngozi iliyodhurika na kuipa uhalisia ngozi yako, jinsi ya kuthibitisha hilo chukua juisi ya chungwa ya baridi paka usoni kaa nayo kwa dakika10 kisha osha uso wako then utaona matokeo.
KAROTI; Ni tunda ambalo hutumika kama kiongo katika chakula,hili husaidia kuzuia saratani hasa zitokanazo na uvutaji wa sigara ( saratani ya mapafu), pia hushusha kolestro katika damu na huzuia ukosefu wa choo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni