Label kubwa ya muziki nchini, WCB ya Diamond Platnumz, a k aT Baba Tiffah huwenda ikamsaini msanii mkongwe wa muziki nchini Q Chief anaetamba na wimbo wa "Sungura"
Muimbaji huyo aliyewahi kufanya vizuri sana na wimbo wa 'Si Ulinikataa’ hivi karibuni alitembelea katika ofisi za WCB na kufanya mazungumzo na uongozi wa label hiyo.
“Tayari nimenza kuyaa approach makampuni makubwa sana,” alisema Q Chief. “Kuna uwezokano nikasaini na mmoja ya wadogo zangu ambaye anafanya vizuri kuliko msanii yeyote hapa nchini,”
Aliongeza, kuwa “Lakini si nasaini kwa sababu mimi ni mjinga, nasaini kwa sababu nataka kuudhihirisha mimi ni Abubakar Katwila na hakunaga Abubakar Katwila mwingine,”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni