Jumamosi, 7 Januari 2017

MWAKA 2017 NISHA ANARUDI KWENYE MOVIE


Muigizaji wa filamu za vichekesho Salma  Jabu ama anaejulikana kama 'Nisha'  amesema mwaka ulipita alifanya filamu chache, na muda wake mwingi kutumia kuimarisha zaidi biashara zake.
"Mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka wangu wa biashara tofauti na movie, kwasababu nimefanya biashara  huku  movie nikiipa muda mchache sana, yote hayo  nilifanya ili kuweka msingi ili niingize kipato bila  kutumia 'NISHA'. Kwasababu kuna maisha baada ya movie na pia umri unazidi kwenda "
Muigizaji huyu ambaye anafanya biashara ya vipodozi na nguo, amedai kuwa alikuwa anaweka mazingira ya biashara zake zikae safi kwa kuwa hawezi kutegemea kuigiza maisha yake yote
"Na mwaka 2017 ndio mwaka wa kuliziba ufa kwenye filamu na Nishasfilm Production, na no timeto waste na drama" alisema Nisha 
So mashabiki wa Nisha wasubiri movie kali kutoka Nishasfilm Production.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni