Kuwa na afya bora ni msingi wa kila binadamu, ili uweze kufikia na kufanikiwa malengo inakulazimu uwe na afya bora, endapo kama afya yako itakuwa mbovu kamwe hauwezi kufikia mafanikio hayo unayoyatarajia, kwasababu unapokuwa na afya bora inakupa nguvu ya kuishi maisha bora wakati wote na kukuwezesha wewe kukamilisha mambo mengi bila kuteteleka.
Kuna msemo unapendwa kutumiwa sana usemao "Mwili haujengwi kwa matofauli" ndiyo afya yenyewe inayozumngumziwa hapo kwamba mazoezi yana umuhimu sana katika afya yetu kwa maisha tunayoishi sasa, vyakula tunavyokula ndio vinavyoweza kutuamulia afya zetu ziweje kwa sasa na baadae.
Wengi huwa wanafanya mazoezi bila kufahamu yanafanya kazi gani kwenye mwili, kuna faida nyingi za kufanya mazoezi ambazo mazoezi haya yanatusaidia sana kujenga afya zetu kuwa imara na kuendelea kuishimaisha bora.
- Mazoezi ya mwili husaidia kuruhusu damu nyingi za kwenda sehemu zote za mwili, na kufanya miguu na mikono ipate joto.
- Mazoezi hukufanya kuwa na nguvu nyingi na kukuepusha kupatwa na uchovu wa kimwili, na kimawazo haraka.
- Pia yanasaidia ubongo kutengeneza dawa ambayo inakupa wewe hali ya kujisikia vizuri, na kukuongezea ustahimilivu wa maumivu.
- Mazoezi yanaondoa mambo yote nikimaanisha mkzo wa mwili pia mfadhaiko wa moyo na kukusaidia wewe uwe unajisikia vizuri maisha yako yote.
- Yanasaidia kuweka rangi ya uso wako, na kukufanya wewe kuwa katika hali nzuri kimwili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni