Jumatano, 11 Januari 2017

SANAMU LA LIONEL MESSI LIMEVUNJWA

Sanamu la mchezaji maarufu  wa Argentina na Barcelona, anayejulikana kwa jina  Lionel Messi limekutwa limevunjwa na watu wasiojulikana likiwa limebakia na sehemu ya chini ya kiuno huku sehemu nyingine ikiwa  haipo kabisa.


Sanamu hilo lililopo mji wa Buenos Aires, Argentina lilijengwa kwa ajili ya kumshawishi Messi kurejea katika timu ya taifa baada ya kutangaza kustaafu, limekutwa likiwa nusu na bila kufahamu aliyefanya tukio hilo.
Serikali ya jiji la Buenos Aires imesema kuwa tayari wameanza kufanya maandalizi ili kulijenga tena sanamu hili liweze kurejea kama ilivyokuwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni