Jumamosi, 7 Januari 2017

BABA YANGU ALIATHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA- HEMEDY PHD

Utumiaji wa madawa ya kulevya ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu na tumepoteza nguvu kazi za taifa nyingi na  huleta madhara makubwa sana kwenye familia, hata katika familia ambazo hujawahi fikiria kama ingekutokea.

 n  

Muimbaji na Muigizaji Hemedy Phd amedai kuwa baba yake mzazi ni mmoja ya watu walioathirika na madawa ya kulevya.
" Baba yangu aliathirika na madawa ya kulevya na tulijitahidi sana kumtibu zaidi ya mara 6 lakini ikashindikana" alisema Hemedy Phd.
"Mara ya mwisho tukagundua wewe mwenyewe unatakiwa uwamue kutoka moyoni kwamba utaka kuchana na madawa ya kulevya"
Pia alikanusha  tetesi zilizosambaa kwamba yeye nae ni mtumiaji wa madawa ya kulevya 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni