Ijumaa, 13 Januari 2017

MAJANGA YAMKUTA SOULJA BOY AKIJIANDA NA PAMBANO NA CHRIS BROWN

Wakati wa maandalizi ya pambano lake la ngumi kati ya Chris Brown, majanga yameanza kumkuta rapper Soulja Boy.


Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Jumanne hii nyumba ya rapper huyo iliyopo Hollywood Hills ilivamiwa na mwizi aliyefanikiwa kuondoka na fedha kiasi cha $10,000, pamoja na vitu vyenye thamani ya $12,000.

Hata hivyo imedaiwa kuwa kamera zilizofungwa katika eneo hilo zimefanikiwa kupata picha ya mwizi huyo ambapo polisi wanaendelea na umfuatiliaji. 
Japo kumekuwa na mvutano juu ya pambano lake na Chris Brown lakini hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuwa wizi huo umefanywa na watu wa upande wa Chris kama kumchanganya Soulja 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni