Jumatano, 11 Januari 2017

DULLY SYKES KUACHIA WIMBO YAKE MPYA


Msanii mkongwe wa muziki nchini, Prince Dully Sykes anajipanga kisawa sawa kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Yono’ baada ya kufanya vizuri sana kwa wimbo  wake wa Inde ambao alimshirikisha  Harmonize wa WCB


“Mungu akipenda kesho naachia mkwaju wangu mpya wimbo unaitwa Yono, chorus ya wimbo nilipewa na Jose Chameleone toka mwaka 2003 baada ya kuipenda nikamwambia akaniruhusu kuitumia,” alisema Dully.
Pia aliongeza, Kwamba   mashabiki wangu wote  wakae mkao wa kula kwa sababu kazi iko poa sana i, pia itatoka pamoja na video yake kwa sababu kila kitu kipo tayari yaani tumejipanga,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni